9/08/2024

SIMBA YAACHANA NA KOCHA JUMA MGUNDA

SHARE
SIMBA YAACHANA NA KOCHA JUMA MGUNDA

Uongozi wa klabu ya Simba umeachana na Kocha Juma Ramadhani Mgunda baada ya mkataba wake kutamatika.

Uongozi wa Simba umetoa Shukrani Kwa Kocha Mgunda kwa utumishi wake ndani ya Simba SC (Simba Senior Team) kisha kuhamishi

wa timu ya Wanawake (Simba Queens) huku kote akitimiza majukumu yake.

Katika kipindi chake Kocha Mgunda ameiwezesha Simba Queens kurejesha taji lake la ligi kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL).

Kwa taarifa hiyo Simba Simba Queens kuanzia sasa itakuwa chini ya Kocha msaidizi, Mussa Hassan Mgosi ambae tayari ameshaanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu ambayo itaanza hivi karibuni.
SHARE

Author: verified_user