9/19/2024

SIFA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

SHARE
Karibu Nijuze Habari Blog, chanzo chako kikuu cha habari zote ndani na nje ya nchi.

Nijuze Habari Blog tumejitolea kukupa habari bora zaidi, tukitilia mkazo habari za Michezo, Ajira, Magazeti, Matokeo, Selection, Interview, Internship pamoja na Makala Mbalimbali.

SIFA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)
UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JWTZ

UANDIKISHAJI

Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: -

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
  • Awe hajaoa/hajaolewa
  • Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
  • Awe na tabia na mwenendo mzuri
  • Awe na akili timamu na afya nzuri

MASHARTI YA UTUMISHI

Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.

Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.

MAAFISA

Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board) huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools).

Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.

MAJUKUMU YA MSINGI YA JWTZ

  • Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.
  • Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.
  • Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoajiwakati wa maafa.
  • Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  • Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.
SHARE

Author: verified_user