RATIBA YA TRENI ZA SGR DAR TO DODOMA 2024
Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu Umma kuwa huduma za awali za usafiri wa treni za abiria katika reli ya kiwango cha kimataifa - SGR kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma zinatarajiwa kuanza tarehe 25 Julai 2024.
Kuanza kwa huduma za treni za SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma kutapelekea mabadiliko ya ratiba za treni kama ifuatavyo;
Treni ya Haraka (Express Train) itatoka Dar es Salaam Saa 12:00 asubuhi na itatoka Dodoma Saa 11:30 asubuhi.
Treni ya kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma itatoka Dodoma Saa 11:30 jioni na itatoka Dar es Salaam Saa 12:55 iioni.
Treni ya kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro itatoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi na saa 10:00 jioni, itatoka Morogoro Saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.
RATIBA KAMILI YA TRENI ZA SGR DAR TO DODOMA TAZAMA HAPA CHINI!
