9/07/2024

RACHID TAOUSSI KOCHA MPYA AZAM FC

SHARE

RACHID TAOUSSI KOCHA MPYA AZAM FC

Klabu ya Azam FC imemtangaza, Rachid Taoussi raia wa Morocco kuwa kocha wake Mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua mikoba ya Youssouph Dabo aliyeondoshwa klabuni hapo.

Kabla ya Azam FC, Taoussi amewahi kuvifundisha vilabu vya Raja CA, RS Berkane na FAR Rabat vya Morocco.

Vingine ni ES Setif na Olympique Khouribga vya Algeria pamoja na timu za taifa za vijana za Morocco.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC, kocha huyo amekuja na wasaidizi wake watatu, ambao ni kocha msaidizi, Ouajou Driss, kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui.

SHARE

Author: verified_user