9/17/2024

NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 MJI BUNDA

SHARE
NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 MJI BUNDA
NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 MJI BUNDA

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda anawatangazia Watumishi
wa Umma wote nafasi ya kazi kwa ajili ya shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.

NAFASI INAYOTANGAZWA
  • Mwandikishaji wa Wapiga kura
SIFA ZINAZOTAKIWA
  • Asiwe na dhamana au Uongozi katika chama chochote cha siasa
  • Awe ni Mtumishi katika Utumishi wa Umma (Public Service)
  • Awe mwadilifu
SIFA ZINAZOTAKIWA
  • Barua zote ziandikwe kwa mkono
  • Barua iandikwe majina kamili yanayotumika katika Utumishi
  • Barua itaje nafasi ya kazi unayoomba
  • Barua itaje cheo katika Utumishi wa Umma
  • Barua itaje Kituo cha kazi
  • Barua iwe na anuani kamili ikiwa na namba ya simu inayopatikana wakati wote. Barua iambatishwe na maelezo (CV).
  • Barua ziwasilishwe kwa mkono masijala ya wazi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/09/2024.

Barua ya maombi iandikwe kwa;
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI,
HALMASHAURI YA MJI WA BUNDA, S.L.P 219,
BUNDA MARA.
SHARE

Author: verified_user