KAMPUNI ya Ulinzi ya West Security, Yenye Ofisi Zake Mbezi Makonde/bagamoyo Road, Inatangaza Nafasi Za Kazi Ya Ulinzi Kwa Watanzania Wenye Sifa Zifuatazo:-
- Awe na Elimu ya Darasa la Saba na Kuendelea.
- Awe na Afya Nzuri.
- Awe na Umri wa Kuanzia Miaka 20 hadi 45.
- Asiwe na Takwimu Zozote za Makosa ya Jinai.
- Awe na Urefu wa Futi 5.7 Kwa Mwanaume na 5.5 Kwa Mwanamke.
MAHITAJI:-
- Barua ya Maombi ya Kazi ya Ulinzi Iliyoambatanishwa na Picha ndogo (Passport Size) tatu za Rangi.
- Barua Mbili za Wadhamini, Kila Mmoja Ikiwa imeambatanishwa na Picha ya Mdhamini, moja ndogo ya Rangi.
- Barua ya Uthibitisho wa Makazi toka Serikali ya Mtaa Anakoishi Mwombaji na Wadhamini.
- Nakala za Vyeti vya Shule au Chuo
- Nakala ya Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA (Kwa Mwombaji na Mdhamini).
Barua zote za Maombi ya Kazi, ziletwe kwa Afisa Mwajiri wa West Security Ltd, S.L.P 79675, Dar Es Salaam - Tanzania.
Kwa Maelezo Zaidi Piga Simu Namba Zifuatazo:-0652-787979, 0753-007607 na 0782-275356
Wahi Haraka, Nafasi Ni Chache.