9/16/2024

NAFASI ZA KAZI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 MANYONI DISTRICT COUNCIL

SHARE
NAFASI ZA KAZI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 MANYONI DISTRICT COUNCIL
NAFASI ZA KAZI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 MANYONI DISTRICT COUNCIL

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni anawatangazia Watumishi Umma wote nafasi za kazi kwaajili ya shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

NAFASI ZINAZOTANGAZWA
✅Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kituo
✅Afisa Mwandikishaji wa Wapiga kura

SIFA ZINAZOTAKIWA
  • Asiwe na dhamana au Uongozi katika chama chochote cha siasa Awe ni Mtumishi katika Utumishi wa Umma (Public Service) 
  • Awe mwadilifu
NAMNA YA KUANDIKA BARUA
  • Barua zote ziandikwe kwa mkono
  • Barua iandikwe majina kamili yanayotumika katika Utumishi
  • Barua itaje nafasi ya kazi unayoomba
  • Barua itaje cheo katika Utumishi wa Umma
  • Barua itaje kituo cha kazi
  • Barua iwe na anuani kamili ikiwa na namba ya simu inayopatikana wakati wote
  • Barua iambatishwe na maelezo (CV)
Barua ziwasilishwe kwa mkono masijala ya wazi ya Mkurugenzi Mtendaji Manyoni
Barua iandikwe kwa;
Msimamizi wa Uchaguzi,
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,
S.L.P 60, MANYONI

Mwisho wa kupokea barua hizo ni tarehe 17 Septemba, 2024 siku ya Jumanne saa 9:30 Alasiri.
SHARE

Author: verified_user